Atunukiwa shahada ya uzamivu akiwa na miaka 78

 


Diborah Chepkisich Lotodo, ameingia kwenye vitabu vya historia nchini Kenya, baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani ya Ushauri wa Kisaikolojia, akiwa na umri wa miaka 78.

Lotodo, alitunukiwa shahada hiyo na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki (CUEA) nchini Kenya, katika mahafali ya taasisi hiyo, yaliyofanyika hivi karibuni katika eneo la Lang’ata jijini Nairobi.

Safari ya masomo ya Lotodo, ambaye ni mjane wa waziri wa zamani wa nchi hiyo, Francis Polisi Loile Lotodo, ilitatizwa mara kadhaa na changamoto za kifedha pamoja na majukumu ya ndoa na kifamilia.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi