CAF wabadilisha tena Mwamuzi atakayechezesha fainali ya AFCON


Shirikisho la soka la Afrika CAF limefanya mabadiliko ya mwamuzi wa mechi ya fainali ya AFCON 2019 kati ya Senegal na Algeria zikiwa zimepita saa 24 tangu wamtangaze mwamuzi wa Afrika Kusini Victor Gomes kuwa ndiye atakayechezesha mechi hiyo.

Shirikisho hilo sasa limemtangaza Mwamuzi Neant Alioum kutoka Cameroon kuwa ndiye atakayeshika filimbi hapo kesho.

Mwamuzi huyo ambaye jana ametimiza umri wa miaka 37, alichezesha mechi ya ufunguzi ya michuano hii kati ya Misri na Zimbabwe.