Hiki ndicho anachokifanya Nape kwasasa


Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amefunguka kuwa yupo jimboni kwake anaendelea na shughuli za maendeleo.

Nape ambaye ni Katibu Mstaafu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, ametoa maelezo hayo leo ikiwa ni siku moja tangu ziibuke sauti mitandaoni zinazodhaniwa kuwa ni yake na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

''Niko jimboni nakagua utekelezaji wa ahadi na kuboresha maisha ya wana Mtama,'' amendika Nape kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kuvuja kwa sauti zinadaiwa kuwa ni ya Nape na Mzee Kinana kunakuja siku chache baada ya Mzee Kinana na Makamba kutoa waraka wakieleza kukerwa na mtu anayejiita mwanaharakati ambaye wamemshutumu kuwa amekuwa akiwachafua bila kuchukuliwa hatua za kisheria.