Loading...

7/14/2019

Julius Mtatiro afunguka baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli


Mapema hii leo Rais John Magufuli alimteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama Cha wananchi (CUF) Julius Mtatiro, ambaye alitangaza kuhamia CCM mwaka jana.

Kabla ya Mtatito kushika nafasi hiyo, awali ilikuwa ikishikiliwa na Juma Homera ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Akizungumzia uteuzi huo, Julius Mtatiro amesema kuwa amezipokea taarifa hizo akiwa safarini na pia amezipokea kwa mshtuko sana.

"Kwa sababu sikutarajia kwamba naweza kuteuliwa na Rais, unajua ukiteuliwa halafu hukuwa unatarajia unapata mshtuko sana." ameeeleza.

Ameendelea kwa kusema, "Ila ukimaliza kupokea kwa mshtuko hizo taarifa inabidi ukubaliane nazo tu, kwa sababu ni kazi ya umma na hakuna budi kuitumikia".


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger