Kocha wa Morocco ajiuzulu baada ya kushindwa kufurukuta AFCON


Kocha wa timu ya Morocco Herve Renard amejiuzulu baada ya matokeo mabaya wakati wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), ambapo Algeria ilinyakua Ubingwa.

Morocco iliondolewa na Benin kwenye mashindano hayo makubwa Afrika kupitia mikwaju ya Penalti katika hatua ya 16.

Renard ameiongoza timu hiyo tangu mwaka wa 2016 ambapo aliiondoa kutoka nafasi 81 hadi 47 kwenye orodha ya viwango vya ubora soka duniani. Mwaka wa 2018 chini ya ukufunzi wake timu hiyo ilishiriki michuano ya kombe la dunia.