Loading...

7/14/2019

Mhe Ditopile awapa UVCCM Pikipiki, awataka kumsaidia kazi JPM

Mbunge wa Vijana Taifa, Mhe Mariam Ditopile ametoa pikipiki moja yenye thamani ya Sh Milioni 2, kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala lengo likiwa ni kurahisisha utendaji kazi wa Umoja huo katika kueneza mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya Rais Dk John Magufuli.

Mhe Ditopile amesema pikipiki hiyo aliyotoa ni sehemu ya ugawaji wa vifaa anavyoendelea kuvigawa kwa ajili ya kuwarahisishia kazi watendaji wa UVCCM katika wilaya mbalimbali nchini.


" Tunaposema CCM ya kijani tunapaswa kumaanisha kweli, twendeni tukawaeleze wananchi wetu mambo makubwa yanayofanywa na Rais Magufuli, tuwaeleze kuhusu Standard Gauge, Stiglers Gorge, Miradi ya Barabara na namna ambavyo Rais ameboresha sekta ya elimu kwa kugawa bure, jukumu letu vijana ni kuisaidia kazi Serikali yetu," amesema Mhe Ditopile.
Loading...