PICHA: Wananchi wawazuia wabunge Mchinga, watoa jambo linalowasumbua


Mbunge wa jimbo la Mchinga, Hamidu Bobali, amejikuta akisimamishwa na wakazi wa kijiji cha Milola mkoani Lindi ambacho kipo kwenye jimbo lake na wananchi hao kutoa kero zao mbali mbali.

Mhe. Bobali akiwa ameongozana na wabunge wengine wanne akiwemo Mussa Mbarouk (Tanga Mjini), Vedastus Ngombale Mwiru (Kilwa Kaskazini), Rukia Kassim (viti maalum Pemba) na Rehema Migilla (viti maalum Tabora), miongoni wa kero ambazo zimetolewa na wakazi wa kijiji hicho ni ukosefu wa huduma ya kituo cha afya.



Wakazi hao wametoa kero hiyo huku wakidai kuwa katika kijiji hicho kimekuwa na zahanati ndogo ambayo inatumika kwa sasa imekuwa ikizidiwa na wagonjwa wengi.

Hata hivyo mbunge Bobali amefafanua suala hilo kwa kudai kuwa tayari mifuko ya saruji iligaiwa kwenye kijiji hicho lakini tatizo ni baadhi ya viongozi wasiokuwa waaminifu wamegawana mifuko hiyo.