Mwanamuziki nyota wa R and B R.Kelly baada ya kuzuiliwa kwa mara nyingine akituhumiwa kuuza wanawake wenye umri mdogo kwa ajili ya ngono atarajiwa kufikishwa mahakamani Jumanne Julai 23 kwa aijli ya kusikilizwa kama ana haki ya kupewa dhamana.
Kutokana na tuhuma zinazomkabilia msanii , mahakama ya Chicago imemnyima dhamana .
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 51 amekumbwa na tuhuma kemkem za unyanyasaji wa ngono.
Kwa upande wake msanii huyo anadai kuwa ni njama dhidi yake.