Raia 17,161 wa Iran wauawa na makundi ya ugaidi


Jumla ya raia 17,161 wa Iran wameuawa na makundi ya kigeni ya ugaidi katika kipindi cha miongo minne (miaka 40) iliyopita.

Hayo yamebainishwa na balozi wa nchi hiyo katika shirika la Umoja wa Mataifa (UN),  Majid Takht Ravanchi akilihutubia baraza la Umoja wa Mataifa (UN).

“Katika kipindi cha miongo minne iliyopita, raia 17,161 wa Iran pamoja na maafisa 200 wakuu wa serikali, ikiwemo rais mmoja, waziri mkuu mmoja, mkuu wa mahakama, wabunge 27 miongoni mwa wengine wameuawa na makundi ya kigeni ya ugaidi,” amesema.