Rasmi: Mzee Kilomoni afurushwa ndani ya Simba SC



Hatimaye Simba SC wametangaza rasmi kumuondoa kwenye sehemu ya baraza la wadhamini la klabu hiyo, Mzee Hamisi Kilomoni.

Uamuzi huo umetangazwa leo na  CEO wa Simnba SC, Crescentius Magori mbele ya waandishi wa habari baada ya Mzee huyo kuvutana sana na uongozi uliopo madarakani sasa kuhusu mabadiliko ya uendeshaji wa timu.

“Hapa karibu tumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu Hamis Kilomoni kuwa mdhamini wa klabu yetu ya Simba. Hamisi Kilomoni ambaye alikuwa ni mdhamini wa Baraza la Simba, amekuwa akipita kwenye vyombo vya habari akieleza habari za klabu yetu," amesema.

Ameendelea kwa kusema, "Kuanzia leo tunatangaza kuwa Mzee Kilomoni sio tena mdhamini wa Baraza la Simba na mkataba wake haupo tena, maana mkataba ulikamilika October 2017. Na kwa msisitizo zaidi maswala yake tumeyafunga leo hatutaliongelea tena suala zaidi hatua za kisheria zitafuata.”