Loading...

7/14/2019

TAMWA yawataka Waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele katika mapigano dhidi ya Udhalilishaji na ukatili wa kijinsiaNa Thabit Hamidu, Zanzibar.

Wanaharakati wa kupinga vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji Nchini wamewataka waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele katika kuandika habari zinazofichua vitendo vya  Udhalilishaji wa kijinsia na ukatili wa wanawake na watoto.

Kauli hiyo imetolewa na Dk Salum Ali Mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) wakati akitoa tathimini kwa wadau juu ya utafitili unaoangazia hali halisi ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili katika wilaya 5 za Unguja Pemba.

Utafiti huo umefanywa na Chama cha Waandishi wa habari wanawake Nchini (Tamwa) na wanaharakati mbalimbali wa kupinga unyanyasaji,udhalilishaji na ukatili kwa  Wanawake na Watoto nchini.

Dk Salimu alisema kuwa katika utafiti huo ambao waliifanikiwa kuwahoji waandishi wa habari na vyombo vya habari  wamebaini kuwa bado kuna uchache wa kuandika na kuripoti habari za udhalilishaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya wananwake na watoto nchini.

Alisema kuwa kwa waandishi mmoja mmoja nao wameuwa nyuma katika kuandiaka habari hizo kutokana na sabababu mbalimbali moja ufinyu wa bajeti kufika katika maeneo husika.

“Tulipokwenda kuuliza katika baadhi ya vyombo tumebaini kuwa wapo waandishi wachache ambao waandika habari hizo lakini wanashindwa kutumia source wengi katika kushibisha habari zao” alisema Dk Salimi kutoka Suza.

Alisema kuwa waandishi wa habari waliowengi wamekuwa  nyuma katika kuandika na hata wale wanaoandika huwa hawazimalizi hadi mwisho kesi za udhalilishaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Kwa wale wanaoandika habari hizi katika utafiti tulioufanya tumebaini kuwa hizo habari zinaishia njiani mfano kesi mbali mbali huripotiwa mwanzo na kati mwisho wa kesi zile hatujui zimefikia wapi” alisema Dk Salim Ali kutoka Suza.
Loading...