UPDATES: Yaliyojiri baada ya Injinia msaidizi MV Mapinduzi kujinyonga


Na Thabit Hamidu, Zanzibar

Injinia Msaidizi wa Umeme katika Meli ya Mv. Mapinduzi II Haji Abdallah Khatibu(55) leo majira ya Saa 4:00 Asubuhi amekutwa amejinyonga katika Meli hiyo huku chanjo cha kujingonga kwake kikiwa bado hakijulikana.


Tukio hilo lilitokea wakati Meli hiyo ikifanya safari zake za kawaida kutoka Unguja saa Moja kamili za Asubuhi na ikitarajiwa kufika Pemba majira ya saa saba adhuhuri.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo  mbele ya  Waandishi wa Habari Katibu Mkuu  Wizara ya Ujenzi  Mawasiliano na Usafirishaji  Zanzibar Mustapha Abdu Jumbe alisema kuwa wamepokea taarifa za tukio hilo lilitoea waati mei ikiwa katika eneo la tumbatu kuelekea isiwani Pemba na uamuru safari isitishwe na meli ilirudi bandarini Unguja kwa Uchunguzi zaidi wa Tukio hilo.

“Tulipo pokea tu Taarifa kutoka wa Kaptein wa mei hiyo Abuubakari Mzee kama Serikali tumeamua kusitisha safari hiyo na kuamuru irudi bandarini unguja kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo” alisema Mustapha Abdu Jumbe.

 Aliongeza kusema kama Seriali tuliamua kusitisha safari hio kutokana na marehemu huyo ni mkaazi wa unuja laini pia idara na vitengo muhimu wa uchunguzi vipo Unguja hivyo wamewahisha uchunguzi wa ina wa tukio hilo.

 Aidha alisema kuwa mara baada ya uwasili kwa mwili huo katika bandari ya malindi Unguja Maafisa kutoka jeshi la Polisi Unguja na vitengo vya upelelezi walifanikiwa kuingia katika chumba kilichotokea tukio hilo na kuchukua vieleezo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

 “Maafisa kutoka Jeshi la Polisi walikuwa 4 ambao ni kitengo cha upelelezi na maafisa 2 kutoka shirika la bandari na usafiri wa baharini Zanzibar ambao wote hao waiingia kwa ajili uchunguzi na wamefanikiwa upiga picha ya tukio jinsi waivyomkuta marehemu huyo”alifafanua katibu Mkuu huyo Mustafa Abdu Jumbe.

Alisema mara baada ya hapo mwili wa marehemu huyo umepelekwa atika hospitai ya rufaa ya mnazi mmoja kwa ajili ya taratibu nyingine kuendelea.

“Ninachotaka kuongeza uwa kifo chake si cha kawaida ndo maana jeshi la polisi limefika kwa ajili ya uchunguzi na watakapo kamilisha nadhani kama kuna haja ya kueleza kwa wanahabari watakuja kuuambieni ila ya wangu ni hayo”alisema katibu huyo.

 Meli hiyo ilikuwa inasafiri na jumla ya abiria 485 na ikioongozwa na Keptein Abuubakari Mzee.