Klabu ya West Ham imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa klabu ya Eintracht Frankfurt Sebastien Haller kwa mkataba wa miaka mitano ambao usajili huo umeweka rekodi kwenye klabu hiyo ya West Ham.
Inaelezwa kuwa Haller, ambaye anakipengele cha kuongeza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, ameigharimu West Ham kitita cha £45m.