Akaunti ya Twitter ya muanzilishi wa Twitter yadukuliwa, Chuckling Squad wahusishwa


Wadukuzi kila kukicha wamekuwa wakiwatesa watum8iaji wamitandao ya kijamii sio bongo tu tena hasa watu maarufu zaidi.

Mwanzilishi na mkurugenzi wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Jack Dorsey amedukuliwa akaunti yake ya mtandao huo.

Hata hivyo Kundi la wadukuzi linalojiita Chuckling Squad limedai kuhusika na udukuzi wa akaunti hiyo ya Jack Dorsey. Akaunti hiyo yenye watu zaidi ya milioni nne, ilianza kutumiwa kwa kusambaza taarifa za chuki na kibaguzi kwa kutumia lugha chafu kwa karibu dakika kumi na tano.

Twitter inasema mitambo yake haikufikiwa na wadukuzi na badala yake kulaumu kampuni ya mawasiliano ambayo haikuitaja jina lake kwa kusababisha hitilafu hiyo.

“Nambari ya simu inayohusishwa na akaunti hiyo ilitumiwa kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyosababishwa na kampuni hiyo ya mawasiliano,” imesema taarifa iliyotolewa na Twitter.

“Hali hiyo ilitoa fursa kwa watu wasio na idhini ya kutumia nambari hiyo kuanza kutuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter.”

Chanzo cha habari kutoka Kampuni hiyo ilithibitishia BBC kuwa wadukuzi walitumia mfumo unaojulikana kama “simswapping” kuchukua udhibiti wa akaunti ya Twitter ya Bw. Dorsey.

Huu ni mfumo ambao inatumiwa kuhamisha nambari halisi ya simu ya Dorsey katika laini nyingine- na kuanza kuitumia.

Wadukuzi mara nyingine hutoa hongo kwa wahudumu wa kampuni za mawasiliano au kuwapotosha kupata namabari halisi.

Kwa kuchukua udhibiti wa nambari hiyo wadukuzi waliweza kuandika ujumbe moja kwa moja katika akaunti ya Twitter ya Bw. Dorsey.

Japo siku hisi watumiaji wengi wa mtandao huo wanatumia programu tumishi kwenye simu zao kutuma ujumbe, awali Twitter ilibuniwa katika mfumo wa kutuma ujumbe mfupi- hali inayoisaidia kudhibiti idadi ya maneno mtumiaji anastahili kuandika.

Wadukuzi waliandika nini?

Ujumbe wa chuki na wa kibaguzi – ulitumwa moja kwa moja kwa kutumia akaunti ya @jack, na wengine waka sabaza ujumbe huokwa kutumia akaunti zingine.

Ujumbe mmoja uliashiria kuna bomu limetegwa katika makao makuu ya kampuni hiyo.

Chuckling Squad imewahi kuhusika kudukua Twitter ya mmiliki wa Blog maarufu ya masuala ya urembo James Charles na watu wengine.