Asilimia 66.3 ya vifo nchini Honduras vyatokana na ugonjwa wa Dengue


Shirika la Afya la Pan American (PAHO) limeripoti karibu asilimia 66.3 ya vifo kutokana na virusi vya ugonjwa wa dengue nchini Honduras huku vifo hivyo vikiwa kati ya watoto chini ya miaka 15.

Wizara ya  afya nchini hadi sasa imethibitisha vifo 89 vya ugonjwa wa dengue tangu Januari.

"Kati ya vifo 89 vilivyothibitishwa, asilimia 66.3 walikuwa chini ya miaka 15, na kwa kweli, tunasikitika sana," Piedad Huerta, mwakilishi kutoka PAHO, aliwaambia waandishi wa habari.

Honduras imekuwa katika tahadhari taifa tangu Julai 2 Rais Juan Orlando Hernandez alisema na kuongeza kuwa kuenea kwa dengue hivi karibuni kulitokana na hali iliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.