Msanii wa muziki nchini, Aslay amewaacha katika mtihani mashabiki zake, baada ya kuonesha kama ana ujio wa kazi mpya kati yake na mkali wa Bongo Flava, AliKiba
Aslay kupitia ukurasa wake wa Instagram, amewachokoza mashabiki wa muziki wake baada ya kuweka picha akiwa studio na Alikiba pamoja na wasanii wengine wa Kings Music.
Hata hivyo bado haijajulikana kama Aslay amefanya ngoma na Alikiba au wasanii wa Kings Music.
Aslay aliweka hivi "Eti Tuanze AUDIO au VIDEO????"
