Mwanadiplomasia Mkuu wa Umoja wa Ulaya amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran hayawezi kutolewa muhanga kuwa sehemu ya hatua ya Marekani yakuwa na makubaliano mapya mapana ya kiusalama na Iran.
Rais wa Marekani wiki hii alisema huenda akakutana na rais wa Iran Hassan Rouhani hivi karibuni kujadilli mzozo unaoendelea kupanuka kati ya mataifa hayo mawili.
Lakini Rouhani anataka vikwazo vya kiuchumi vilivyowekewa nchi yake viondolewe kabla ya mazungumzo hayo kufanyika.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema makubaliano yaliyonuiwa kuizuwia Iran kumiliki silaha za nyuklia ni makubaliano yaliyoyashirikisha mataifa tofauti yanayoendana na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kwamba kile kilichoko kwa sasa kinahitaji kuhifadhiwa.
Mogherini amesema masuala mengine yanayohitaji kufanyiwa kazi yanayoheshimu makubaliano hayo yataungwa mkono.