Mawaziri wa Umoja wa Ulaya watoa onyo dhidi ya Brexit isiyokuwa na makubaliano

Mawaziri wa Umoja wa Ulaya wameihimiza Uingereza kuchagua kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya yaani Brexit kwa utaratibu mzuri, huku baadhi yao wakionesha wazi wasiwasi juu ya hatua ya Waziri Mkuu Boris Johnson kusitisha kwa muda vikao vya bunge, hali inayozidisha hatari ya mpasuko zaidi wa kisiasa nchini humo.

Wakati Mawaziri wa mambo ya kigeni na wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya wakikutana mjini Helsinki serikali ya Johnson ilitoa changamoto kwa wapinzani wake ndani ya bunge la Uingereza ama waiangushe serikali hiyo au kubadilisha sheria kusimamisha safari ya Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31.

Waziri Mkuu wa Uholanzi Stephan Blok amesema bado wana matumaini kwamba itawezekana kuzuwia Brexit isiyokuwa na makubaliano.

Bunge la Uingereza limepinga mara tatu makubaliano ya kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya yaliyokubaliwa kati ya Waziri mkuu wa Zamani Theresa May na Umoja huo.
Mpya zaidi Nzee zaidi