Fountain Academy Dodoma yatambulisha jeshi lake tayari kwa ligi daraja la pili


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

Timu ya Fountain Academy ya Jijiji Dodoma inayoshiriki daraja la pili Tanzania bara SDL, imetambulisha rasmi kikosi chake cha wachezaji 28, ambacho kitashiriki ligi hiyo kwa msimu huu2019/ 2020.

Zoezi hilo pia limeenda sambamba na utambulisho  wa jezi zao mpya watakao zitumia kwa msimu huu wa ligi hiyo.

Timu hiyo ambayo inamilikiwa na Shule ya kulea vipaji  vya mpira wa miguu Fountain Academy ambayo inatimu za umri wa chini ya miaka 13, 15, 17 na timu kubwa ambayo inashiriki ligi daraja la pili na timu ya wasichana ya Fountain Queens.

Jezi zilizotambulishwa kwa msimu ujao ni  jezi nyeusi kwa michezo ya nyumbani na nyeupe kwa michezo ya ugenini katika ligi hiyo.

Katika tukio la utambulisho wa timu yao ulienda sambamba na michezo mbalimbali ikiwamo mchezo wa timu ya Fountain Academy ya umri wa chini ya miaka 15 iliyocheza na wenzao ya umri Kama huo ya BQ Contractors ya Dar es saalam.

Na Fountain kufungwa bao moja kwa sifuri, mchezo wa pili ulikuwa kati ya BQ Contractors ya umri ya chini ya miaka 17 walicheza Makole Academy, na BQ Constractors kushinda kwa bao mbili dhidi ya moja la Makole Academy.

Na mchezo wa mwisho ulikuwa wa timu kubwa ya Fountain Academy ambayo walicheza na timu ya Area C ambayo pia inashiriki ligi daraja la pili SDL na timu hizo kutoshana nguvu kwa kutokufungana.

Mara baada ya mchezo huo kocha msaidizi wa Fountain Academy Robart Kasiga, amesema vijana wake hawakucheza kwa kiwango chake kutokana na kuingia na tation kubwa katika mchezo huo.

Amesema makosa yote aliyoyabaini atahakikisha anayafanyia kazi kabla ya ligi hiyo kuanza kwani anaamini timu yake ni nzuri na inacheza mpira wa kufundishwa na hana wasiwasi juu ya ushiriki wa ligi hiyo.

"Hatujacheza kwa kiwango cheti kutokana na wachezaji wetu kuingia katika mechi na ration lakini naamini timu yangu ni nzuri na kabla ya ligi hiyo kuanza nitahakikisha makosa yote niliyoyaona nayarekebisha" amesema Kasiga.

Mmiliki wa timu hiyo Japhet Makau amesema lengo la kuanzisha timu hiyo ni kuhakikisha nchi inafika mbali katika mpira wa miguu hivyo wao Kama wadau ameona aanzishe Academy ambayo itasaidia kukuza vipaji hapa nchini na kufika mbali katika maswala ya mpira.