Loading...

8/13/2019

Galatasaray kuzungumza na Tottenham kuhusu kumsajili Victor Wanyama


Siku nne baada ya kipindi kirefu cha uhamisho nchini Uingereza kufungwa, ripoti kutoka nchini Uturuki zinasema kuwa mmoja kati ya viungo wakabaji Mkenya, Victor Wanyama anayechezea timu ya Tottenham Hotspur na Mfaransa Tiemoue Bakayoko kutoka Chelsea wako kwenye rada ya Galatasaray.

Tovuti ya Sport Witness inasema kuwa afisa kutoka Galatasaray, Sukru Haznedar yuko jijini London kwa mazungumzo. Kocha Mauricio Pochettino alipendezwa na soka ya Wanyama na kumleta Southampton mnamo Julai mwaka 2013 na kisha Tottenham Juni mwaka 2016.

Hata hivyo, baada ya nahodha huyo wa Harambee Stars kukosa kucheza mechi nyingi kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya magoti katika msimu hiyo miwili iliyopita, kocha huyo kutoka Argentina alionyesha kumshiba Wanyama aliposaini viungo Tanguy Ndombele na Giovani Lo Celso.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger