Loading...

8/13/2019

Umaarufu wa Prince Harry washuka tangu alipokutana na mkewe Meghan


Kiongozi wa chama kinachounga mkono kujiondoa kwa Uingereza katika Muungano wa Ulaya Nigel Farage amewakosoa wajumbe wa familia ya ufalme wa Uingereza, akiumuelezea marehemu mama yake Malkia kama mwenye uzito wa kupita kiasi ,mvutaji sigara na mnywaji wa vileo vikali .

Pia amesema kuwa kiwango cha umaarufu wa mwanamfalme Harry au Duke of Sussex kimeshuka tangu alipokutana mkewe, Meghan.

Kiongozi huyo ametoa kauli yake alipokuwa akihudhuria kikao cha vuguvugu la mrengo wa kulia nchini Australia. Hata hivyo, Msemaji wake amekanusha taarifa kuwa Bwana Farage alimuita Mwanamfalme Harry Mwanamfalme anayejali ubaguzi wa rangi.

Lakini amethibitisha kuwa Bwana Farage alitoa kauli ambazo zilirekodiwa wakati wa mkutano kuhusu hatua za siasa za kihafidhinia mjini Sydney Jumamosi.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger