Loading...

8/13/2019

Majeruhi Wanane kati ya 46 wa ajali ya Moto Morogoro wafariki


Majeruhi Wanane kati ya 46 wa ajali ya lori la mafuta lililoteketea kwa moto, waliopokewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamefariki ndani ya siku ya jana na juzi.

Taarifa aliyotiwa saini na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa MNH, Aminiel Aligaesha inaeleza miili Saba imerudishwa Morogoro isipokuwa mmoja wa Amani Keneth Urio (26) wa Moshi – Marangu, unahifadhiwa MNH.

Wengine ambao miili yao imerejeshwa Morogoro na miaka yao ya umri katika mabano ni Jaclspm Elian Shao (25), Kulwa Dominic (28), Ismail Ally Mwanga (28), Muhidin Maulid Mtingwa (42), Maige Hamis(20), Issa Kasawa Mussa (35) na Adinani Khamis (-). .

Wagonjwa 25 wanajitambua na 13 hawajitambui wapo chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). .

Baadhi ya majeruhi waliopo ICU na umri wao kwenye mabano ni Saidi Ally Maulidi (29) anatoka Mafisa, Khalfan Juma Iddy (26)- Msamvu,  Omary Abdallah (24) Msamvu, Joseph Yowana Lewanga (48)-Mafisa na ndugu yake wa karibu ni Riziki Changulu.

Wengine ni Ramadhan Yusuph Mdoe (50)-Mwembesongo, Aloyce Gwerina Mpozi (36) - Kihonda, Mussa Ally Athumani (28) – Mtawala na ndugu yake wa karibu ametajwa kuwa ni Juma Ally na Ramadhani Ally (Chande (26) ambaye haijafahamika anakotokea wapi.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger