Idadi ya Wachina wanaokwenda kutalii Marekani yazidi kupungua


Mkurugenzi mkuu wa Idara ya utalii ya taifa ya Marekani, Christopher Thompson amesema, China siku zote ni chanzo muhimu sana cha watalii kwa utalii wa Marekani.

Mwaka jana matumizi ya watalii wa China nchini Marekani yalishika nafasi ya kwanza, lakini idadi ya wachina wanaotalii nchini Marekani imeonesha mwelekeo wa kupungua, ambao unaendelea kupungua tangu mwaka huu.

Thompson amesema, siku zote wanafuatilia mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, kwa sababu inaleta athari mbaya kwa sekta ya utalii.

Takwimu zilizotolewa na serikali ya Marekani zinaonesha kuwa, mwaka jana idadi ya wachina waliokwenda kutalii nchini Marekani imepungua kwa asilimia 6 ikilinganishwa na ya mwaka juzi, ambayo imepungua kwa mara ya kwanza katika miaka 15 iliyopita.