Trent Alexander Arnold afukuzia rekodi ya Mesut Ozil


Beki wa kulia wa Liverpool Trent Alexander Arnold anafukuzia rekodi inayoshikiliwa na Mesut Ozil wa Arsenal katika Ligi Kuu nchini Uingereza.

Mpaka sasa Trent Alexander Arnold amefanikiwa ku-assist kwenye mechi tano mfululizo za ligi kuu, akifanya hivyo mara ya mwisho dhidi ya Norwich katika ushindi wa 4-1 akimpa assist Divock Origi.

Record ya assist nyingi mfululizo inashikiliwa na Mesut Ozil, ambae ana rekodi ya ku-assist mara 7 mfululizo. Inategemewa Arnold atakaribia kuifikia rekodi hiyo kwenye mechi ijayo ya Liverpool dhidi ya Southampton.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items