Iran yafanya jaribio la kombora

Jeshi la Walinzi Iran limetangaza kwamba limefanikiwa kufanya jaribio jipya la kombora.

Kulingana na Shirika la serikali la Iran Tesnim, kamanda wa jeshi  la nchi hiyo ametangaza kuwa kombora limefanyiwa majaribio mapya kwa mafankio.

Akisema kwamba Iran inaendelea kujaribu majeshi kadhaa ya ulinzi na ya kimkakati,

"Hizi ni hatua ambazo zinaongeza nguvu ya taifa let. Jana ilikuwa moja ya siku zenye mafanikio makubwa" alisema kamanda huyo.

Selami hakutoa habari juu ya aina ya kombora lililofanyiwa majaribio.