Tammy Abraham ampa ushindi wa kwanza Frank Lampard

Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, ameweza kufunga magoli mawili na kuiwezesha timu yake kuondoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Norwich kwenye dimba la Carrow Road.

 Goli jingine la Chelsea lilifungwa na  Mason Mount na yale ya Norwich yalifungwa na Todd Cantwell pamoja na Teemu Pukki.

 Ushindi huo wa Chelsea unakuwa ni wa kwanza kwa kocha Frank Lampard akiiongoza klabu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.