Japan yafunguka kuhusu uamuzi wa Korea Kusini

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema uamuzi wa Korea Kusini kufuta makuabaliano ya kubadilishana taarifa za kijasusi unaaharibu uaminifu kati ya nchi hizo mbili, na akaapa kushirikiana kwa karibu na Marekani ili kuleta amani katika kanda hiyo.

Akizungumza kabla ya kuanza mkutano wa kundi la nchi saba tajiri duniani G7 utakaofanyika Ufaransa kuanzia kesho, Abe pia ameikosoa Korea Kusini kwa kutotimiza ahadi zake za nyuma.

 Makubaliano ya kijeshi kati ya nchi hizo yalianza mwaka 2016. Korea Kusini imesema ilifanya uamuzi huo kwa sababu Japan iliishusha hadhi ya kibiashara ya Korea Kusini, ambayo inasema ilibadilisha ushirikiano wa usalama kati ya nchi hizo.

Korea Kusini inasema itaishusha hadhi ya Japan pia, mabadiliko ambayo yataanza kutekelezwa Septemba.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items