Kocha wa Juventus kukosa mechi mbili za mwanzo


Klabu ya Juventus imethibitisha kocha wao mkuu Maurizio Sarri hatakuwa kwenye benchi katika mechi zao mbili za kwanza za Serie A dhidi ya Parma na Napoli kufuatia kuendelea na ugonjwa wa Pneumonia ambao amegundulika anao hivi karibuni.

Timu sasa ipo chini ya benchi lake la ufundi.

Pneumonia ni maambukizi ambayo yanaweza kusababisha mapafu kujaa majimaji au usaha, na pia huleta homa, baridi kali, na kupumua kwa shida. Hivi karibuni Sarri alithibitsha kuwa kwa wastani huwa anavuta sigara 60 kwa siku moja.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items