Loading...

8/16/2019

Kocha wa Liverpool athibitisha Golikipa wake mwingine kuumia


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp leo amesema kipa wake Adrian yupo katika hatihati ya kukosa mechi ya kesho dhidi ya Southampton baada ya kuumizwa kifundo cha mguu na shabiki aliyevamia uwanjani katika mchezo wa UEFA Super Cup dhidi ya Chelsea juzi Jumatano.

Tukio hilo lilitokea wakati wachezaji wa Liverpool wakishangilia baada ya Adrien kuokoa penati kuwapa ushindi, shabiki huyo aliingia kuungana nao lakini akateleza wakati mlinzi wa uwanjani akijaribu kumkamata na kugongana na wachezaji kadhaa.

Tayari Liverpool wanamkosa kipa wao namba moja Allison Becker ambaye anasumbuliwa na maumivu ya shavu la mguu, hivyo kama Adrian hatacheza kesho, kocha Jurgen Klopp amesema anaweza kuwatumia makipa wa akiba Andy Lonergan na Caoimhin Kelleher.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger