Nchi ya Luxembourg iliyopo bara la Ulaya inatarajiwa kuwa nchi ya kwanza barani Ulaya kuhalalisha uzalishaji na matumizi ya bangi.
Wizara ya Afya Nchini humo imeelezea mipango ya kupitishia sheria ambayo itaifanya nchi hiyo kuwa ya kwanza kuhalalisha matumizi ya Bangi barani Ulaya, Imesema kuzuia kila kitu ndiko kunawavutia vijana wengi kujaribu.
Iwapo Sheria itapitishwa wenye umri kuanzia miaka 18 wataweza kununua bangi kisheria kwa ajili ya matumizi binafsi (Kujiburudisha)
