Hali ya lishe kwa wanawake walio katika umri wa uzazi wa miaka 15 hadi 49 mkoani Dodoma hairidhishi ambapo wanawake wawili kati ya kumi wanakabiliwa na utapiamlo hali inayochangia kwa kiasi kikubwa vifo vitokanavyo na uzazi kabla na baada ya kujifungua.
Aidha asilimia 19 ya wajawazito wanatajwa kutotumia chumvi yenye madini joto hali inayoathiri afya ya mtoto kwani ambapo anaweza kuzaliwa akiwa na udumavu wa ubongo au wa viungo.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kondoa Msoleni Dakawa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma wakati wa zoezi la utoaji elimu kuhusu matumizi ya lishe bora kwa afya ya mama na mtoto katika Kata ya Kingale wilayani humo.
Meneja mradi wa lishe kutoka shirika lisilo la kiserikali la Save The Children, Benety Malima amesisitiza umuhimu wa mama mjamzito kuzingatia lishe kabla na baada ya kujifungua.
