Polisi wakanusha kumkamata Mwandishi wa Habari


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Zuberi Chembela amekanusha taarifa za kukamatwa kwa mwandishi wa habari za kichunguzi Bollen Ngetti, anayedaiwa kukamatwa jana Agosti 8 na kupelekwa kituo cha polisi cha Stakishari.

 Kamanda Chembela amesema, hana taarifa za kukamatwa kwa mwandishi yoyote yule wa habari katika kituo hicho cha Stakishari na kwamba amekuwa akipigiwa simu zinazohoji kukamatwa kwa mwandishi huyo mara kadhaa kitu ambacho si cha kweli.

''Hakuna taarifa za kukamatwa kwake, hafu wiki mbili tatu zilizopita nilipigiwa tena simu kuulizwa juu ya huyo huyo mwandishi Bollen Ngetti kama sisi tunamshikilia, niliwauliza hizo taarifa mmezitoa wapi, niliambiwa eti kwenye mitandao ya kijamii, mimi sina taarifa hizo ila wacha nifuatilie ili nijue kama Bollen Ngetti ni kweli yupo Stakishari'' amesema  kamanda Chembela.

Taarifa za kukamatwa kwa mwandishi huyo zilianza kusambaa siku ya Agosti 8, kwa madai ya kwamba amekamatwa na askari watatu, na kupelekwa kituo cha polisi Stakishari.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items