Mkurugenzi Mwandamizi TAKUKURU akamatwa kwa Rushwa


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemkatama afisa wake aliyekuwa mchunguzi mwandamizi makao makuu Dar es salaam, Cosmas Revelian Batanyita kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kwa wafanyabiashara wawili waliokuwa wakichunguzwa kwa makosa mbalimbali likiwemo la ukwepaji wa kodi.

Mkurugenzi wa TAKUKURU, CP Diwani Athumani amesema afisa huyo kwa sasa amefukuzwa kazi na leo anakabidhiwa rasmi kwa Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) ili hatua za kimahakama ziendelee.

Katika hatua nyingine amesema kuwa Tanzania imeshika nafasi ya kwanza kati ya nchi 35 zinazopambana na rushwa barani Afrika, huku akielezea kwamba utafiti huo umefanywa na mashirika ya kimataifa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items