Mahakama yatupilia mbali maombi ya aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa


Mahakama ya Rufani imetupilia mbali maombi ya marejeo ya aliyekuwa Mkuu Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Mwaka 2016, Bageni aliwasilisha maombi ya marejeo mahakamani hapo akiiomba mahakama hiyo ibadilishe uamuzi wake.

Uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo ya Bageni ulioandaliwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo waliosikiliza maombi hayo, umetolewa leo, Jumatano, Agosti 14, 2019 na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani, Elizabeth Mkwizu.