Seneta Marekani: Trump ameshindwa vita dhidi ya Iran


Seneta wa Marekani wa chama cha Democrats, Chris Murphy, amesema Rais Donald Trump “ameshindwa vita hivi” dhidi ya Iran, akieleza kuwa kuendelea kwa mapigano kunaidhoofisha Marekani huku ikiifanya Iran kuwa na nguvu zaidi.

“Marekani imedhoofika. Iran imeimarika,” Murphy alisema katika mahojiano na NBC. Alisema angeunga mkono hata “makubaliano mabaya” iwapo yangewezesha kumaliza vita na kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.

Murphy alisema gharama na changamoto za kuufungua tena Mlango huo muhimu wa kimkakati zinazidi kuongezeka, huku mazungumzo ya kutafuta suluhu yakiwa yamekwama.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi