Maofisa Ardhi waliosimamishwa kuchunguzwa, Serikali yatoa siku 30


Serikali imetoa Siku 30 kufuatia kusimamishwa kwa maofisa ardhi 183 wa Wizara ya Ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kufanyika uchunguzi kwa watendaji hao waliowafutia wateja madeni ikiwemo kupunguza saizi ya ukubwa wa viwanja kupitia mfumo wa malipo na kuisababishia serikali hasara ya mapato yatokanayo na viwanja.

Baada ya uchunguzi wale watakaobainika kutenda makosa hayo hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao huku wale ambao hawatakutwa na makosa watarejeshwa Kazini.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na  Waziri Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi ,amesema kuwa timu ilioundwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa watendaji waliohujumu mfumo wa ulipaji malipo ya viwanja itawajumuisha Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) pamoja na taasisi nyingine ambazo zina wataalamu wanaohusika na mifumo inayotumia mitandao.

Hata hivyo amesema kuwa uchunguzi wa timu hiyo utafanyika kuanzia miaka mitatu yani 2016/hadi 2019 ambapo mfumo huo wa kulipia viwanja ulianza kutumika.

Lukuvi amesema kuwa watendaji waliosimamishwa kazi wamebainika ndani ya miezi sita ya mwaka wa fedha 2018/19 ambapo mfumo wa malipo Hazina ndio umepeleka wao kubainika kwa sababu unaonyesha moja kwa moja.

“Naomba muelewe hawa waliosimamishwa hivi sasa ni wale walioiibia serikali kuanzia sh laki moja na kuendelea,lakini katika uchunguzi utakaofanywa hata kama umeiibia serikali sh moja utachukuliwa hatua za kisheria,” amesema Lukuvi.

lengo la kutoa siku hizo chache za uchunguzi ni kutokana na kwamba ushahidi wa mfumo unaonyesha kila kitu kwa hiyo hakuna sababu ya kutumia muda mrefu kufanya uchunguzi.

“Nimesikia malalamiko yakuwa waliosimaishwa wanasema watu wamewaibia password zao,si kweli hayo ni mawazo yao walijisahau kama mfumo wa malipo wa Hazina unaonyesha Moja kwa Moja ndicho kilichowakamatisha,” amesisitiza Lukuvi.

Aidha amewataka waliobaki nao wajiandae na zoezi hilo maana baada ya uchunguzi kuna majina mengine yatabainika kwa sababu wanaanzia kuchunguza tokea mfumo ulipoanza kutumika.

Akitolea mfano wa kiwanja kilichopo mkoani Mbeya ambacho kilikuwa Na square Mita 20,234 lakini katika.mfumo amejaziwa square Mita 502 ambapo amekuwa akilipa sh 63,000 kwa.mwaka badala ya sh mil sita  kwa mwaka jambo ambalo ameisababishia Serikali hasara ya sh milioni million 68 tokea kipindi hilo hadi hivi sasa.

Hata hivyo Lukuvi amesema kuwa walioshirikiana na watendaji wa Wizara hiyo kufanya mchezo huo wasifikiri wako salama bali watalipa kiasi cha fedha ambacho amefutiwa deni ikiwemo kupunguziwa ukubwa wa kiwanja ambacho amekuwa akilipa fedha pungufu.

Waziri Lukuvi ametolea ufafanuzi huu ya ulipaji wa tozo za kodi ya hati za majengo alisema  wananchi wanapaswa kulipa ndani ya miezi sita kuanzia Julai mosi hadi Desemba inamaana ukipitisha muda huo itabidi ulipe na faini.

Hatua hivyo aliwasisitiza wananchi kutokwenda kwa afisa Ardhi kwa ajili ya kufanya malipo ya hati za viwanja Na badala yake wanaweza kulipia benki kupitia simu zao za mkononi na  kurejeshewa risiti.

Lukuvi amesisitiza kuwa kuanzia Oktoba mosi mwaka huu huduma zote za upatikanaji wa hati za viwanja zitapatika katika mikoa na kanda kama ilivyokuwa awali ili kuepusha usumbufu kwa wananchi kutoka mikoani kuja Dodoma kufuatilia zoeizi zima la hati.