Na Ahmad Mmow, Lindi
Wafanyabiashara na watumiaji wa bidhaa zinazotengenezwa kwa mbao wameaswa waepuke kununua mbao zizovunwa kwa njia halali.
Wito huo umetolewa leo na ofisa masoko mmsaidizi wa Shirika la Kuhifadhi Mpingo na Maendeleo ( MCDI), Kassim Ulega alipozungumza na Muungwana Blog katika viwanja vya Ngongo, manispaa ya Lindi.
Alisema MCDI ambayo makao makuu yake yapo mjini Kilwa Masoko linatambua juhudi za serikali kulinda misitu. Kwahiyo wananchi na wafanyabishara waunge mkono jitihada hizo kwakununua na kutengeneza samani( fenicha) kutokana na mbao ambazo miti yake inavunwa kwa njia halali.
Alisema wananchi hawana sababu wa kununua, mbao ambozo miti yake imevunwa nje ya mfumo rasmi.
Alisema serikali kwakutambua umuhimu wa mahitaji ya miti imevipa uwezo vijiji kumiliki na kuhifadhi misitu. Ambapo katika vijiji hivyo kuna miti yenye ubora na inayovunwa kwa uvunaji endelevu.
Alisema shirika hilo na mashirika mengine yasio yakiserikali kwa kusaidiana na serikali yamefikisha elimu ya uvunaji na huifadhi wa misitu. Kwahiyo wananchi na wafanyabishara watapata bidhaa zilizotokana na uvunaji halali.
''Pia wawe wazalendo kwanunua bidhaa za ndani zinazotokana na malighafi za ndani. Wanapokalia viti, kulalia vitanda na samani nyingine waanze kujiuliza kama mbao zilizotumika kutengeneza ni halali ama la. Wasipojiuliza hivyo watakuwa wanafurahia uharibifu wa misitu,'' alisema Ulega.
Aliwaasa wananchi watambue kuwa uvunaji haramu unasababisha serikali kupoteza mapato kupitia kodi, uharibifu wa misitu na mazingira unaosababisha mabadiliko ya tabia nchi.
