Na Thabit Hamidu, Zanzibar
Waziri wa Elimu na Mafunzo Zanzibar, Riziki Pembe Juma amesema Serikali ya Mapinduzi imekuwa ikitoa kipaumbele katika Sekta ya Elimu kwa lengo la kujenga na kuimarisha Uchumi wa Nchi na kufikia Uchumi wa kati ifikapo 2020.
Amesema Serikali imekuwa ikiweka mikakati mbalimbali ya kuinua sekta hiyo kwa lengo la kuwaelimisha wananchi na kuchochea Uchumi wa Nchi.
Hayo ameyaeleza leo katika Kongamano la vijana wa CCM ( UVCCM) katika shamra shamra za kuadhimisha siku ya vijana Duniani ambapo Kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdull Wakil kikwajuni, Mjini Magharib Unguja.
Siku ya Vijana Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehr 12 mwezi wa nane 08 ya kila mwaka na Kali mbiu ya siku hii kwa mwaka huu ni " Transform Education, Huku Uvccm wameadhimisha siku hii kwa kauli mbiu isemayo Kulinda na Kujenga Ujamaa.
Waziri Pembe alisema Kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikiweka mikakati Mbali mbali ya kukuza Elimu Nchini na kuinua Uchumi wa Nchi na kufikia malengo waliyojiwekea.
Aliongeza kusema Serikali imeweka mikakati ya kuinua Elimu kama vile Dira ya Maendeleo ya Nchi 2020,Mkuza II na III, Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015/2020 na Sera ya Elimu ya mwaka 2006.
"Sera na mikakati hote hiyo inalenga katika kumuendeleza kijana kupata Elimu bora, Ujuzi,maarifa ili kukabiliana na changamoto mbali mbali za kimaendeleo na kuinua uchumi wa Nchi yetu" alisema Riziki Pembe Juma.
Aidha Waziri Pembe alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi imepiga hatua katika kueneza Elimu kwa ngazi zote na kuimarisha ubora wa elimu na kuwapatia vijana maarifa na Ujuzi wa kuwawezesha kujiajiri.
"Serikali yetu imefanikiwa kutoa Elimu bila ya malipo kwa watoto wote wenye miaka 12 Hari kidato cha Nne bila ya ubaguzi wa aina yoyote" alisema Wazir Pembe.
