Mkurugenzi TBS awasimamisha kazi watumishi wawili


Watumishi wawili wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), ambaye ni Emmanuel Kiwango na mwenzake, Jenifa Jackson wamesimamishwa kazi kituo cha mpaka wa Namanga kwa tuhuma za kuruhusu uingizwaji wa mifuko mbadala isiyokidhi viwango.

Mkurugenzi wa Shirika hilo, Dk Yusuph Ngenya akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,  watu hao ambao ni msimamizi wa kituo hicho kilichopo mpakani wa Tanzania na Kenya.

Amesema kuwa mzigo wa mifuko hiyo mbadala ulikamatwa Agosti 5, 2019 baada ya kupitishwa na wasimamizi wa shirika hilo kituoni hapo wakati wakijua kuwa haikidhi viwango.

Dk. Ngenya amesema kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko ya wananchi kutoka Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro kutokana na kuwepo kwa  utitiri  wa mifuko hiyo mbadala isiyokidhi viwango.

“Nimeamua kuwasimamisha kazi watumishi hawa wakati uchunguzi ukiendelea kufanyika. Inaonekana  kama wameweza kupitisha mifuko hiyo wakati wakijua kuwa haikidhi viwango, ni jambo ambalo wamezoea kufanya hata kwa bidhaa nyingine,” amesema.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items