Loading...

8/14/2019

Mchezaji atimuliwa kwenye timu kisa kipindi cha Televisheni


Gazeti la Ufaransa la L’Equipe limeripoti kuwa Mchezaji wa Adil Rami ametimuliwa katika klabu ya Marseille baada ya kuacha kwenda mazoezini na kwenda kushiriki katika kipindi cha Televisheni cha Fort Boyard.

Mfaransa huyo ameonekana katika show hiyo ambayo walikuwa wakicheza mieleka kwenye matope.
Show hiyo ilirekodiwa mwezi Mei mwaka huu siku ambayo alitakiwa kuwepo mazoezini lakini akasingizia kuwa ni majeruhi.

Marseille hawakujua ukweli huo mpaka pale show iliporushwa kwenye TV Juni 29, na kumwambia Rami asiripoti katika mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya. Sasa imeripotiwa kuwa Marseille wameamua kumtimua beki huyo,33, kwa kosa la utovu wa nidhamu.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger