Migogoro ya ardhi yaibuka tena Kyerwa mchungaji anusurika kuuawa na wananchi



Na Clavery Christian Kyerwa.

Wananchi wa kijiji Kishanda kitongoji Kishanda B Kata Kibale wilaya ya Kyerwa mkoa Kagera wamevamia shamba la mwekezaji na kufyeka miti aina ya pain na kuua mbuzi pamoja kufyeka shamba la migomba wakimtuhumu mwekezaji huyo kulisha mifugo yake mazao yao.

Akizungumza na Muungwana Blog mwenyekiti wa kijiji Kishanda bw, Medius Athanas amesema kuwa tangu mwekezaji huyo apewe eneo hilo kwa ajili ya kufanyia shughuli zake za ufugaji mwaka 2007 amekuwa na migogoro na wanakijiji hicho ambapo ameitwa kwenye mikutano kadha wakadha ya kijiji hicho na kushindwa kuudhuria kitu ambacho kiliwafanya wanakijiji hao kuisi anawadharau na anafanya makusudi kulisha mifugo yake mazao yao hali ambayo imewafanya kumchukia na kufikia hatua ya kujichukulia sheria mkononi.

"Mwaka 2012 wanakijiji walikamata ng'ombe za bw, Triphoni Jeremia mpaka kwenye ofisi ya kijiji wakimtaka aondoe mifugo yake kwa kuwaharibia mazao yao na yeye alikuja akaomba msamaha na wakamsamehe lakini hakujirekebisha" Alisema bwa Medius Athanas.

Muungwana Blog ilipata nafasi ya kuongea na Mchungaji Triphoni Jeremia ambaye ni muhanga wa tukio hilo ambapo yeye amesema kuwa chanzo cha mgogoro huo ni yeye kununua eneo hilo na kuwekeza katika kijiji hicho ambapo amesema kuwa amekuwa akishitakiana na baadhi ya wanakijiji hicho tangu aanze kuwekeza katika eneo hilo ambapo amesena kuwa anadhan walikuwa na mpango wa kumdhurumu mzee aliyemuuzia shamba hilo kwakuwa yeye umri wake umeenda na walipoona amemuuzia mchungaji Triphoni Athanas waliumia sana ndo sababu ya kuanza njama za kumuondoa.

"Mgogo huu ulianza mwaka 2007 wakati nanunua mahali hapa ambapo niliuziwa na mzee John Bugomola Mtekanga aliniuzia kwa usalama ila majirani hawakupenda nafikili walikuwa na mpango wa kumdhurumu huyu mzee na mimi baada ya kununua nikawa nimeweka mifugo yangu hapa ya ng'ombe ambapo asubuhi yake walikuja watu watano na Medius Athanasi akiwemo wakafyeka zizi langu la ng'ombe na kuliweka chini nilitoa taarifa kwenye balaza la aridhi la kata ambapo waliweza kuwakamata na baada ya mwaka mmoja na miezi minne walikuja kuniomba msamaha nami nikawasamehe lakini baada ya hapo Medius Athanasi aliendelea na mgogoro ambapo alikuja akapanda miti ya karitusi kwenye shamba langu ambayo ndo imebaki pale juu haikukatwa" Alisema mchungaji Triphoni Jeremia.

Migogoro ya ardhi na wafugaji imekuwa ikikemewa vikali na serikali ya awamu ya tano lakini bado inaendelea kuibuka mbali na viongozi wa ngazi zote kujaribu kutoa elimu kwa wananchi na kutenga maeneo ya ufugaji na kilimo. Wilaya ya Kyerwa ni moja ya wilaya mkoani Kagera ambayo inakesi nyingi za migogoro ya aridhi.

Jeshi la polisi mkoani Kagera limethibitisha kuwepo kwa tukio hili na limesema kuwa linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Mpya zaidi Nzee zaidi