https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mrajisi awafunda viongozi wa bodi ya Kahawa | Muungwana BLOG

Mrajisi awafunda viongozi wa bodi ya Kahawa


Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Kagera, Robert Makene Kitambo ameutaka uongozi wa bodi ya chama cha ushirika wilayani Ngara kushirikiana na wakulima wa zao la Kahawa kutatua changamoto zinazo wakabili katika zao hilo na kuhakikisha wanalizalisha kwa tija.

Mrajisi huyo amesema hayo leo katika kikao cha kuchagua bodi mpya ya kuongoza chama hicho kufuatia ile iliyokuwepo kumaliza muda wake. Pia ameongeza kuwa ni vema wajumbe wa bodi hiyo kujua kuwa wakulima ndiyo waajiri wao hivyo ni vema kuwatumikia na sio kwenda kuwa juu yao na kusahau majukumu yao yaliyowapeleka hapo.


"Changamoto zilizopo kwenye ununuzi na uuzaji wa zao la kahawa tunazitambua na nimeiagiza bodi ya chama cha Ngara Famers kwenda kuzitatua kero zenu na kuhakikisha mnauza mazo yenu kama serikali inavyoelekeza na kulipwa kwa wakati," amesema Roberty Makene.

Aidha Mrajisi huyo ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inaongea na taasisi za kifedha ili kupeleka huduma za kifedha karibu na mkulima ili kuondoa adha ya kufata mbali malipo yake pale anapokuwa amemaliza kuuza huku akiwaomba wakulima kufungua akaunti za benki ambazo hazina makato makubwa ambapo makato yake ni shilingi elfu tatu (3000) ikiwa ndio riba ya kulinda akaunti.


Aidha amewasisitiza wakulima kuacha mara moja biashara ya kahawa ya magendo kwani mtu akikamatwa anafanya hivyo serikali haitamuonea haya na atakuwa amejiingiza matatizoni bure kwani ni biashara haramu na isiyokubalika.
Ngara famers imefanya uchaguzi wake leo Agosti 31 ambapo imempata mwenyekiti na makamu wake na wajumbe wengine saba watakao iongoza kwa muda wa miaka mitatu.