Mwanamitindo Bongo Ben Breaker atajwa kuwania tuzo za Star QT Afrika Kusini


Mwanamitindo ambaye pia ni dansa hapa Bongo, Ben Breaker amechaguliwa kuwania tuzo kubwa za nchini Afrika Kusini ambazo zitafanyika Oktoba 26, 2019.

Tuzo hizo ambazo amechaguliwa mwanamitindo huyo zinafahamika kwa jina la Star QT.

Katika tuzo hizo Breaker ametajwa kuwania katika vipengele viwili ambavyo ni Best Icon na People's Choice.







Kura za tuzo hizo zinatarajiwa kuanza kupigwa August 14 ya mwaka huu kupitia tovuti ya www.starqt.com/awards.

Kwa mwaka huu itakuwa ni mara ya sita kwa tuzo hizo kufanyika tangu zilipoanzishwa 2014.