NIDA yawataka wananchi kukamilisha vielelezo ili kupata vitambulisho


Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mkoani Morogoro imewataka wananchi mkoani humo kukamilisha vielelezo muhimu vya maombi ya kupata vitambulisho hivyo ili waweze kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Usajili huo unafanywa chini ya mfumo mpya uliowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Ofisa Msajili wa mamlaka hiyo mkoani hapo, James Malimo alisema hayo alipoelezea maendeleo ya kazi ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole kwa Mkuu wa Mkoa, Dk Kebwe Stephen Kebwe.

"Tumesogeza huduma katika ngazi ya kata, tunapeleka namba hizo na mwananchi anaweza kwenda kusajili simu yake,"alisema Malimo.

Hata hivyo, alisema lengo la mkoa wa Morogoro ni kusajili wananchi 300,000 na hadi sasa usajili huo umefikia asilimia 75.