Polisi Uganda wakanusha kudukua mawasiliano ya Bodi Wine


Polisi wa Uganda wametupilia mbali madai yaliyochapishwa na jarida la Wall Street Journal (WSJ) kwamba walitumia kampuni ya mawasiliano ya simu Huawei kudukua mawasiliano ya mwasiasa wa upinzani, Bobi Wine.

Msemaji wa polisi nchini Uganda, Fred Enanga ametaja ripoti hiyo kama ya kupotosha na yenye lengo la kuchafua Jeshi hilo.

 “Tunaamini kwamba ripoti ya WSJ ambayo iliigwa na gazeti la hapa nchini, Daily Monitor inanuiwa kuhujumu idara ya polisi nchini Uganda (UPF) na kunufaisha wanasiasa fulani,” alisema Enanga.

Ameendelea kwa kusema “Inasikitisha kwamba walichagua kiongozi mmoja wa upinzani ilhali kuna wadau wengi wa siasa hapa nchini ikiwemo wanasiasa, wanaharakati, wabunge, wanahabari, miongoni mwa wengine,” alisema.
Mpya zaidi Nzee zaidi