Rais Magufuli amwagiwa sifa za ushindi 2020


Na Timothy Itembe Mara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa(UVCCM)Raymond Mwangwala amewahikikishia wananchi wa Tarime mkoani Mara kuwa Chama chake kitashinda uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020  kwasababu Rais awamu ya Tano John Pombe Magufuli amekipaisha Chama hicho kwa kutekeleza miradi na kusimamia ilani ya CCM ya uchaguzi 2015-2020.


Akizungumza na wanachama wa chama hicho jana katika ukumbi wa hoteli ya CMG Moteli iliyopo Mjini Tarime alisema kuwa hana shaka ya kushinda Chama chake katikia uchaguzi wa seriklai za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi 10 au 11 ,2019 mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2020 kwasababu Rais John Pombe Magufuli anatekeleza miradi mikubwa kwa jamii huku akisimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya uchaguzi2015-2020.

"Niwaombe nduugu zangu kujitokeza kwa wingi kukipigia kura Chama cha mapinduzi katika uchaguzi wa seriklai za mitaa pindi utakapotangazwa na ule uchaguzi mkuu ili kumuunga Riasi wetu kwani anatekeleza miradi kwa wananchi na miradi hiyo ni frusa ya Ajira za mda mfupi ndani ya jamii,ni imani yangu Mimi binafsi nimejenga tabia ya kushinda na wala sio tabia ya kushindwa,"alisema Mwangwala.

Kuhusu Wakenya kuja kujiandikisha katika Daftari la wapiga kura nchini Tanzania Katibu huyo alisema kuwa ni kosa la kisheria Mtu wa Taifa lingine kuja kujiandikisha Nchini hapa kwa lengo la kupiga kura hali sio Raia wa Tanzania na kuwa vyombo vya dola linapaswa kulitazama kwa jicho la upande jambo hilo na kulishugulikia ili kama kuna yeyote alitumia nafasi hiyo kujiandikisha hali sio Raia wa Tanzania vyombo vya ulinzi na usalama vishugulikie.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi mkoani hapa, Jacobo Mangaraye alisema kuwa ndani ya mkoa Mara wanaimani kurudisha majimbo yanayoongozwa na upinzani kama vile jimbo la Tarime Mjini linaloongozwa na Esther Matimo,Tarime Vijijini na jimbo la Bunda Mjininalinaloongozwa na Esther Bulaya.

Mangaraye aliwataka wanachama na wapiga kura kwa ujumla kuunga mkono Rais Magufuli kwani anayanya kazi kubwa  ya maendeleo pamoja na kupiga vita vitendo vya Rushwa pamoja na vya ukatili ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wanachama wake kuondoa tofauti zilizopo na kudumisha mshikamano.

Naye katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya Tarime,Khamisi Mkuruka alisema kuwa uwandikishaji wa uboreshaji wa Daftari la wapiga kura kwa upande wa Tarime zoezi hilo limeenda vizuri licha ya kuwa zilijitokeza dosari ndogondogo na kuwa walizibiti Wakenya waliokuwa na nia ya kuja kujiandikisha katika zoezi hilo.

Mkaruka  aliongeza kuwa ushindi wowote unategemea umoja na mshikamano vinginevyo Wanachama wa Chama cha mapinduzi wilaya Tarime kuna haja kujipanga ili kuhakikisha wanashinda viti vyote vya serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika kati ya mwezi wa 10,11 2019 na uchaguzi mkuu 2020 kuwa wanachama wa chama chake wasijihakikishie ushindi pasipo kufanya kazi ya ziada.