Rais Vladimir Putin wa Urusi ameliamuru jeshi la nchi hiyo litafute jibu linalofaa baada ya Marekani kufanya jaribio la kombora ambalo lilikuwa marufuku kuambatana na makubaliano yaliyobatilishwa hivi karibuni ya kutengeneza silaha za nyuklia.
Katika jaribio la Jumapili iliyopita kombora la nyuklia la Marekani lililofanyiwa ukarabati liliifikia shabaha yake na kupiga umbali wa kilomita zaidi ya 500.
Marekani imesema inabatilisha mkataba huo kwa sababu Urusi imekuwa ikiuwendeya kinyume, madai ambayo viongozi wa mjini Moscow wanakanusha.
Akizungumza hii leo, Rais Putin ameituhumu Marekani kueneza kampeni ya uwongo inayodai kwamba Urusi imevunja maakubaliano "ili kuunganisha nguvu zake na kueneza makombora yaliyopigwa marufuku katika sehemu mbali mbali za dunia.
Ameiamuru wizara ya ulinzi na taasisi nyengine "kuchukua hatua zinazofaa ili kujiandaa kwa jibu linalofaa".