Serikali kufanya mageuzi makubwa kusimamia sekta ya sanaa na ubunifu


Katika kuboresha na kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya Sanaa na Ubunifu (Art and Creative Industry) na kusogeza huduma kwa Wasanii na Wabunifu serikali ya awamu ya tano iko katika mchakato wa kuziunganisha taasisi zinazoshughulika na sekta hii na kuunda mamlaka moja.

Taasisi hizo ni Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu na Chama cha hakimiliki na Hakishiriki (Cosota).

 Kwa msingi huu Wasanii wa aina zote wakiwemo watunzi na waandishi mbalimbali, wabunifu, Waandishi wa habari na wadau wote wa Sanaa mnakaribishwa katika mkutano na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Innocent Bashungwa utakaofanyika Siku ya Jumatano, Tarehe 28/08/2019 katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Center (JNICC) jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 Asubuhi.

Mbali na kujadili kwa kina mchakato wa uundwaji wa mamlaka moja ya kusimamia sekta ya Sanaa na Ubunifu kutakuwa pia na mazungumzo ya gawio la mirabaha kwa kazi za Wasanii wa muziki.