SIDO wafanikiwa kutengeneza Mashine ya kisasa ya kukata Nyama


Na. John Walter, Arusha

Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa  Arusha kupitia kituo chao cha uendelezaji wa Biashara Wamefanikiwa  kutengeneza mashine ya kisasa ya kukata nyama itakayokuwa Mbadala wa Matumizi ya Magogo.

Hayo yamesemwa na Meneja wa SIDO mkoani hapo Nina Nchimbi  wakati wa akizungumza na Muungwana Blog kwenye maonyesho ya 26 ya Kilimo na Mifugo (Nane nane) Njiro Jijini Arusha, ambapo amesema mashine hizo wataziuza kwa wafanyabiashara wa nyama kwenye mabucha kwa bei nafuu ili kila mmoja awe nayo.

Amesema wameamua kutengeneza mashine hiyo kwa kuwa Bodi ya nyama nchini imeshapiga marufuku kukata nyama kwenye Magogo ifikapo Septemba 30 mwaka huu.

Nchimbi amesema  wapo tayari kuwahudumia wajasiriamali  kwa kuwapatia kuwajengea uwezo ili waweze kuanzisha viwanda na kuzalisha bidhaa bora na sahihi kwa mlaji wa Mwisho.

Mbali na hayo, SIDO wameiomba serikali kwa kushirikia na shirika hilo ambalo lipo kila mkoa kutenga maeneo kwa ajili wajasiriamali kwenye halmashauri zote kwa kuwa wapo wajasiriamali wengi lakini wanakabiliwa na uhaba wa maeneo ya kufanyia shuguli zao hali inayowafanya wengine kufanyaia kazi maeneo ambayo sio rafiki.

Kauli mbiu Nane nane mwaka 2019: “Kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi.”