Takriban watu 400 wafariki kwa joto Uholanzi

Shirika la taifa la takwimu nchini Uholanzi CBS, limesema takriban watu 400 zaidi walikufa nchini Uholanzi, wakati Ulaya ilipokabiliwa na joto kali la kuvunja rekodi.

Kwa ujumla watu, 2964 walifariki nchini humo wakati joto hilo lilipoanza tarehe 22 Julai, ambalo ni asilimia 15 zaidi ya namna hali inavyokuwa wakati wa msimu wa kiangazi.

Viwango vya joto vilipanda barani ulaya mwishoni mwa mwezi Julai na kwa mara ya kwanza tangu viwango hivyo kuanza kuwekwa, uholanzi ilifikia nyuzi joto 40 mnamo Julai 25.

Vifo takriban 300 vilivyorekodiwa vinawajumuisha wazee waliyo zaidi ya miaka 80 na watoto wachanga.

Shirika hilo la CBS, limesema vifo vingi vilitokea Mashariki mwa Uholanzi ambako viwango vya joto vilikuwa juu, na hali hiyo ya joto kudumu muda mrefu kuliko maeneo mengine katika taifa hilo lililo na idadi ya watu milioni 17.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items